1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Annan alitaka baraza la usalama kuondoa mkwamo

Sekione Kitojo17 Machi 2012

Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa na mataifa ya Kiarabu ,Arab League, kuhusu mzozo wa Syria ,Kofi Annan ,amelihimiza baraza la usalama la umoja wa mataifa kuondoa mkwamo uliopo ili kumaliza ghasia nchini Syria

https://p.dw.com/p/14Lzf
U.N.-Arab League envoy Kofi Annan reads a statement after his meeting with Syria's President Bashar al-Assad in Damascus March 11, 2012. Annan said he was optimistic after a second round of talks with Assad on Sunday, but acknowledged it would be difficult to reach a deal to halt the bloodshed. REUTERS/Khaled al-Hariri (SYRIA - Tags: CIVIL UNREST POLITICS) // Eingestellt von wa
Mjumbe wa umoja wa mataifa na mataifa ya Kiarabu Kofi AnnanPicha: Reuters

Akihutubia kikao cha faragha cha baraza hilo lenye wajumbe 15 kwa njia ya video , Annan amesema ikiwa kutakuwa na uungwaji mkono imara kwa juhudi zake za kupatanisha ili kufikia kusitishwa kwa mapigano , nafasi itakuwa kubwa zaidi kwake kuweza kumaliza kabisa mapigano. Ujumbe utakaokuwa na nguvu zaidi na umoja , utakuwa ni nafasi nzuri ya kuweza kubadilisha mwelekeo wa mzozo huu, amesema mjumbe katika baraza hilo , akitoa muhtasari wa maelezo ya Annan .

Annan ameeleza kuwa majibu ya Syria kuhusiana na mapendekezo yake ya amani yenye vipekee sita yanavunja moja hadi sasa , lakini kikosi chake bado kinazungumza na serikali ya Syria, amesema mwanadiploamsia huyo.

Annan anahimiza kupatikana usitishaji wa mapigano, upelekaji wa waangalizi na mazungumzo ya kisiasa kati ya serikali na upinzani.

Annan pia amesema katika ujumbe wake kuwa mbinyo wenye mwelekeo wa pamoja ambao umekuwa ukitolewa na baraza la usalama la umoja wa mataifa dhidi ya Syria umefanikiwa hapo kabla , kama vile kuilazimisha serikali ya Syria kuondoa majeshi yake kutoka nchi jirani ya Lebanon. Kuondolewa kwa majeshi hayo kulikamilika mwaka 2005.

Ausschnitt aus: epa03134044 A handout photo made available by the official Syrian Arab News Agency (SANA) shows Syrian President Bashar al-Assad (L) meeting with Alla Alexandrovsaya, chairwoman of the Syrian-Ukrainian Friendship Committee in the Ukrainian Parliament, in Damascus, Syria, 06 March 2012. According to SANA, the meeting took up the recent developments in Syria. EPA/SANA/HANDOUT HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++
Rais Bashar al-Assad wa SyriaPicha: picture-alliance/dpa

Urusi na China mara mbili zimepiga kura ya turufu dhidi ya maazimio ya baraza hilo yanayoishutumu serikali ya rais Bashar al-Assad nchini Syria, kwa juhudi zake zilizodumu mwaka mmoja sasa kuuzima uasi unaodai demokrasia nchini humo. Umoja wa mataifa unasema kuwa mashambulio ya majeshi ya Assad dhidi ya waandamanaji yamesababisha watu zaidi ya 8,000 wengi wao raia kuuwawa.

Majadiliano juu ya mswada wa tatu wa azimio , mara hii ukiandikwa na Marekani na unaotoa wito wa kusitishwa mapigano na kupata nafasi kwa mashirika ya kutoa misaada kupeleka misaada ya kiutu, umekwama kuhusiana na makubaliano juu ya nani nchini Syria kwanza asitishe mapigano na nani alaumiwe kwa kuzusha mzozo huo.

Akizungumza na waandishi habari mjini Geneva baada ya kutoa maelezo hayo, Annan amesema , "Nina matumaini hivi karibuni kuwa mtasikia sauti moja katika baraza la usalama."

Deputy representative of the U.N. Secretary General for Afghanistan, Francesc Vendrell, right, and Ahmad Fawzi, spokesman for the U.N. Special representative for Afghanistan Lakhdar Brahimi talk to each other prior to a joint press conference in the media center inKoenigswinter near Bonn, Wednesday, Nov. 28, 2001, on the second day of the U.N. organized Talks on Afghanistan. (AP Photo/Markus Schreiber)
Msemaji wa mjumbe wa umoja wa mataifa na mataifa ya Kiarabu Ahmad FawziPicha: AP

Balozi wa Syria katika umoja wa mataifa , Bashar Ja'afari, amewaambia waandishi habari kuwa kikosi cha ufundi kutoka katika ofisi ya Anna kitawasili mjini Damascus Jumapili. Msemaji wa Annan , Ahmad Fawzi , amesema kuwa watajadili wazo la kupeleka wachunguzi wa kimataifa nchini Syria.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre

Mhariri: Amina Abubakar