1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika katika magazeti ya Ujerumani

Zainab Aziz Mhariri: Mohammed Khelef      
14 Februari 2020

Yaliyozingatiwa kwenye magazeti ya Ujerumani juu ya Afrika ni pamoja na taarifa kwamba baraza la kijeshi linalotawala Sudan limekubali kumpeleka kwenye mahakama ya kimataifa, ICC aliyekuwa rais wa Sudan Omar al Bashir.

https://p.dw.com/p/3XmQu
Sudan Khartum | Prozess & Urteil Omar al-Baschir, ehemaliger Präsident
Picha: picture-alliance/Anadolu Agency/M. Hajaj

Der Tagesspiegel 

Gazeti la Der Tagesspiegel linasema baraza la majenerali linaloongoza nchini Sudan kimsingi liko tayari kumpeleka Omar Bashir kwenye mahakama ya mjini The Hague kujibu mashtaka ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu..Gazeti la Der Tagesspiegel imemnukulu mjumbe wa baraza la kijeshi la Sudan Mohammed Hassan al Taishi akisema kwamba serikali ya Sudan ipo tayari kushirikiana na mahakama ya mjini The Hague ICC.

Gazeti hilo linatilia maanani uamuzi wa baraza la kijeshi la Sudan kwamba umetokana na matamshi ya waasi wa jimbo la Darfur la magharibi mwa Sudan. Mabadiliko katika msimamo wa baraza la kijeshi la Sudan yanatokana na mazungumzo juu ya kuleta amani yanayofanyika kati ya serikali ya Sudan na makundi kadhaa ya waasi kutoka jimbo la Darfur. Kwenye mazungumzo hayo waasi wameitaka serikali ya Sudan imkabidhi Omar Bashir kwa mahakama ya kimataifa ya mjini The Hague kujibu mashtaka ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Hata hivyo gazeti la die tageszeitung kuhusu mada hiyo linatanabahisha kwamba ni mapema mno kusema iwapo Omar -al Bashir kesho tu atatiwa ndani ya ndege na kupelekwa mjini The Hague.

Neue Zürcher

Gazeti la Neue Zürcher linatupa habari juu ya ziara ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta nchini Marekani. Gazeti hilo linatilia maanani kwamba Marais Kenyatta na Donald Trump walizungumzia juu ya mkataba wa biashara lakini linauliza jee Marekani inataka biashara tu Kenya? 

Siyo jambo la ajabu kwamba rais Kenyatta amefanya ziara nchini Marekani na kufanya mazungumzo ya biashara na rais Donald Trump. Tangu miaka miwili iliyopita utawala wa Trump umekuwa unazungumzia juu ya kumpata mshirika wa Marekani barani Afrika. Mnamo mwaka 2004  Morocco na Marekani zilitialiana saini mkataba juu ya biashara huru. Kenya itakuwa nchi ya kwanza kusini mwa jangwa la Sahara kufikia mkataba wa biashara na Marekani tangu Trump aingie madarakani.

Hata hivyo gazeti la Neue Zürcher linatilia maanani kwamba Marekani inalenga shabaha ndefu zaidi barani Afrika.Mkataba na Kenya ni kituo cha kwanza cha kuiunganisha Marekani na nchi nyingine za Afrika katika juhudi za nchi hiyo za kuzuia ushawishi wa China barani Afrika.

Die Welt

Gazeti la Die Welt linatupasha habari juu za mwanaharakati maarufu wa nchini Angola Rafael Marques de Morais aliyeunga mkono ziara ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel aliyoifanya nchini Angola wiki iliyopita. Mwanaharakati huyo amenukuliwa na gazeti Die Welt akisema juu ya mabadiliko ya uongozi.

Watu hawaelewi kwamba yaliyotokea nchini Angola ni mabadiliko katika kiti cha rais na siyo mabadiliko katika chama tawala. Hakuna serikali mpya. Chama ni kile kile kinachoendelea kutawala tangu miaka 45 iliyopita. Rais mpya Joao Lourenco ni kiongozi mwenye dhamira ya kuleta mabadiliko lakini  amenasa katika mfumo ule ule wa chama. Mwanaharakati Rafael Marques de Morais wa nchini Angola amenukuliwa na gazeti la Die Welt akisema anaunga mkono anayofanya rais Joao Lourenco hasa kuhusu kuwachukulia hatua mafisadi wakubwa waliojitajirisha wakati wa utawala wa rais Dos Santos.

Vyanzo./ Deutsche Zeitungen