Afrika kama mbia wa kiuchumi | Matukio ya Afrika | DW | 18.05.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Afrika kama mbia wa kiuchumi

Licha ya ustawi wa nguvu wa kiuchumi, Afrika bado siyo muhimu katika biashara ya nje ya nchi za Ulaya: Na ili kuibadilisha hali hiyo, wawakilishi wa kiuchumi kutoka Afrika na Ulaya watakutana mwishoni mwa mwezi wa Mei.

Wajasirimali wa Ujerumani wanaopendelea kushirikiana na Afrika wameungana katika chama cha uhusiano baina ya Ujerumani na Afrika. Idadi ya wanachama wa chama hicho inazidi kuongezeka, na sasa imefikia mia saba. Miongoni mwa wanachama hao ni kampuni kubwa za kimataifa, kama Siemens na ThyssenKrupp. Mwenyekiti wa chama cha uhusiano baina ya Afrika na Ujerumani, Stefan Liebig, amelalamika kwamba kampuni zisizokuwa na habari za kutosha juu ya Afrika zinaliepuka bara hilo kutokana na kulinasibisha na migogoro. Mbali hilo, ushindani sasa umekuwa mkali zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali kutokana na shuhguli za China, Brazil na India barani Afrika. Kutokana na ushindani huo wajasirimali wa Ujerumani wanahitaji mikakati mipya. Hayo ameshauri mwenyekiti huyo Liebig. „Anachokisikia mtu barani Afrika kote ni kwamba teknolojia na bidhaa za Ujerumani zinathaminiwa sana. Lakini pia inapasa kusema kwamba bidhaa za Ujerumani aghalabu ni ghali."

Kinachotakiwa: Bidhaa za bei nafuu

--FILE--Chinese engineers from the Zhongyuan Petroleum Exploration Bureau (ZPEB) of Sinopec and Sudanese engineers read engineering drawings in Sudan, Africa, 24 October 2010. Southern Sudan vowed in October that Chinas huge investments in its oil sector would remain safe, whatever the outcome of the regions January 9 independence referendum. Pagan Amum, secretary general of the regions ruling Sudan Peoples Liberation Movement (SPLM), said ties between Beijing and the south were very good, following talks with a delegation of senior leaders from Chinas ruling Communist Party. The largest investment in southern Sudan today is Chinese. They have invested billions of dollars in the oil sector, and have a large number of Chinese workers in the oil fields, said Amum. We have given assurances to the Chinese leadership delegation to protect the Chinese investments in southern Sudan, and are desirous to see more investment in the future, he added, speaking in the southern capital of Juba. Sudan is the third largest oil producer in sub-Saharan Africa, with more than 80 percent of known oil reserves thought to lie in the south, while China is the biggest importer of the oil.

Ushindani rahisi: China inatoa huduma nafuu

Sambamba na bidhaa mahsusi kwa mahitaji ya nchi za Afrika, nchi hizo pia zinapendelea miradi ya kubalidishana taaluma. Anaepeleka teknolojia barani Afrika pia atapaswa kutoa mafunzo kwa waafrika. Mfano ni katika sekta ya nishati endelevu. Nchini Nigeria miradi hiyo inajenga msingi wa ugavi imara wa nishati, kama anavyosisitiza Waziri wa sayansi na utafiti wa Nigeria, Ita Okon Bassey, ambae hivi karibuni alifanya ziara nchini Ujerumani: „Ama kwa hakika tunajaribu kuanzisha ushirikiano nchini Ujerumani na mashirika ambayo hasa ya uhusiano na chuo kikuu cha Stuttgart na vyuo vingine vya Ujerumani. Nafikiri hayo yanajenga mazingira yanaowawezesha washirika wa Nigeria kuja Ujerumani na kujifunza tekinolojia."

Kinachodhamiriwa: Uzalishaji ndani ya nchi yenyewe

Volkswagen-Mitarbeiterin Mandisa Jacobs bringt am Samstag (19.06.2010) im Volkswagen-Werk im südafrikanischen Uitenhage bei Port Elizabeth ein VW-Emblem auf der Heckklappe eines VW Polo an. VW beschäftigt an dem Standort etwa 5600 Mitarbeiter. Etwa 100.000 Fahrzeuge werden jährlich produziert, ca. 40.000 davon sind für den Export bestimmt. Foto: Friso Gentsch/Volkswagen

Waajiriwa zaidi ya 5000: Volkswagen Afrika Kusini

Nchi za Afrika hasa zinasisitiza juu ya kushughulikia ndani ya bara hilo, sehemu kubwa ya sekta ya kuongeza thamani ya bidhaa. Hayo yana maana kuwa kazi zitafanywa na waafrika wenyewe, katika sekta ya zana ufundi na kushuhgulikia mali ghafi. Kampuni ya Ujerumani, Siemens, imejipanga kuona utaratibu huo ukiongezeka kati ya asilimia 80 na 90 nchini Ghana, Nigeria na Angola.

ARCHIV - Ein Bus fährt aus dem Atomkraftwerk Koeberg, 40 km von Kapstadt entfernt (Archivfoto vom 24.02.2006). Südafrikas einziges kommerzielles Atomkraftwerk ist nach einer Pannenserie abgeschaltet worden. Nachdem am Montag bereits die erste Reaktorblock wegen eines technischen Problem heruntergefahren werden musste, folgte nach Rundfunkangaben vom Samstag der zweite Block am Freitagabend. Ursache war ein Defekt im Kühlsystem des Generators. Beide Einheiten des bei Kapstadt gelegenen Koeberg-Atomkraftwerks haben zusammen 1800 Megawatt Leistung. Vor zwei Jahren hatte ein vergessener Bolzen in einem Generator zur Abschaltung des Kraftwerks und damit in der Region zu tagelangen Stromausfälle geführt. EPA/NIC BOTHMA +++(c) dpa - Bildfunk+++

Kogezo Afrika Kusini: Nigeria pia inataka nishati ya kinyuklia

Sambamba na nishati endelevu nchi za Afrika pia zinakodolea macho ufundi ambao hata nchini Ujerumani hakuna anaeutaka tena. Katika ziara yake ya hivi karibuni nchini Ujerumani, waziri wa nishati wa Nigeria aliifafanua mipango ya nchi yake ya nishati ya nyuklia. Pia katika sekta hiyo Ujerumani ni mshirika anaethaminiwa, amesema waziri huyo.

Mwandishi: Mösch, Thomas.

Tafsiri: Mtullya, Abdu

Mhariri: Othman, Miraji