Afisa wa zamani wa riadha Okeyo afungiwa maisha michezoni
31 Agosti 2018David Okeyo amepigwa marufuku kushiriki katika uongozi wa chama hicho maisha baada ya kupatikana na hatia ya kuchukua mamia kwa maelfu ya dola za malipo ya ufadhili kwa matumizi yake binafsi.
Okeyo, katibu mkuu wa zamani na makamu wa rais wa chama cha Riadha nchini Kenya AK, pamoja na kuwa mjumbe wa baraza la shirikisho la vyama vya riadha duniani IAAF, na Joseph Kinyua, mweka hazina wa zamani wa chama hicho, walikuwa wakichunguzwa na bodi ya maadili ya michezo kuhusiana na malipo yaliyofanywa na kampuni ya vifaa vya michezo ya Marekani Nike kati ya mwaka 2003 na 2015.
Katika hukumu iliyomo katika kurasa 74 na kutolewa leo Alhamis, bodi hiyo iligundua kwamba katika nyakati kadhaa Okeyo hakuweza kukieleza chama hicho cha Riadha cha Kenya kutolewa kwa fedha zilizotolewa na kampuni ya Nike alikofanya kutoka katika akaunti ya benki ya chama cha riadha na pia hakuweza kuonesha ushahidi wowote juu ya matumizi ya fedha hizo.
Kwa hiyo amepatikana na hatia ya kukiuka maadili mara 10 baada ya kuchukua fedha hizo za ufadhili ambazo "zingeweza kuelekezwa katika kusaidia maendeleo ya mchezo huo wa riadha nchini Kenya" na kuondolewa kutoka katika nafasi yake katika baraza la IAAF.
Kinyua alikutikana na bodi hiyo "kufanya tabia kama hiyo" lakini hakuwa afisa wa IAAF katika wakati huo, ilionekana kwamba hafungwi na sheria hiyo ya maadili katika wakati huo na kwa hivyo ameepuka adhabu.