Afisa mkuu mtendaji wa IEBC achukua likizo kujiweka pembeni wakati wa uchaguzi | Media Center | DW | 20.10.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Media Center

Afisa mkuu mtendaji wa IEBC achukua likizo kujiweka pembeni wakati wa uchaguzi

Mkurugenzi mtendaji wa tume ya uchaguzi nchini Kenya, ambaye upande wa upinzani ulitaka ang'atuke kabla ya uchaguzi wa rais kuitishwa upya Oktoba 26, amesema hii leo anakwenda likizo kwa wiki tatu. Ezra Chiloba anasema ameamua mwenyewe kuchukua likizo ya wiki tatu. hatua hiyo itamuweka pembeni wakati uchaguzi wa rais utakapofanyika.

Tazama vidio 01:45
Sasa moja kwa moja
dakika (0)

Serikali ya Madrid yaungwa mkono na Merkel pamoja na wakuu wengine wa Umoja wa Ulaya katika mjadala wa Catalonia kutaka kujitenga. Video mpya yaonesha mji wa raqqa ukiwa umeharibiwa sana kufuatia vita vya wiki kadhaa kati ya majeshi yanayosaidiwa na Marekani dhidi ya wanamgambo wa IS. Kansela Angela Merkel aanzisha mazungumzo kamili ya kuunda serikali ya muungano. Na maafisa wa polisi nchini Marekani waanzisha uchunguzi dhidi ya muandaaji filamu Harvey Weinstein kufuatia madai ya baadhi ya wanawake kuwa aliwadhalilisha kingono