Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 23.08.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Afghanistan

Uchunguzi utafanywa kujua kama wanajeshi wa nchi shirika wanahusika na kuuliwa raia zaidi ya 70 nchini Afghanistan

Kabul:


Vikosi vya nchi shirika vinavyoongozwa na Marekani nchini Afghanistan, vimeamua uchunguzi ufanywe baada ya wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan kusema hujuma za mabomu za vikosi shirika zimegharimu maisha ya raia 76 magharibi ya nchi hiyo.Rais Hamid Karzai amelaani kile alichokiita "kifo cha mashahidi zaidi ya 70,wengi wao wakiwa wakiwa wakinamama na watoto."Viokosi vya nchi shirika vinavyoongozwa na Marekani vilisema jana  waasi 30 wameuliwa akufuatia mapigano pamoja na vikosi vya usalama vya Afghanistan na vikosi vya kimataifa vikisaidiwa na helikopta za kivita katika mkoa wa Shindand.Serikali ya Marekani pia inatilia shaka taarifa ya serikali ya Kaboul."Tuhuma zote kuhusu kuuliwa raia wasiokua na hatia zitachunguzwa kwa makini.Vikosi vya nchi shirika vinafanya kila liwezekanalo kuwaepushia hasara ya maisha raia.Uchunguzi utafanywa."Taarifa ya vikolsi hivyo vya kimataifa imesema hii leo.Maandamano yameitishwa kulaani mauwaji hayo huko Shindand.Waandamanaji wamebeba mabango dhidi ya rais Hamid Karzai na dhidi ya kuwepo vikosi vya nchi shirika nchini humo.

 • Tarehe 23.08.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/F3So
 • Tarehe 23.08.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/F3So
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com