AFCON: Cameroon yaingia fainali | Michezo | DW | 03.02.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Kandanda

AFCON: Cameroon yaingia fainali

Cameroon imeichapa Ghana mabao mawili kwa bila na kujihakikishia nafasi katika fainali ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON. Cameroon itakuwa inawania ubingwa kwa mara ya tano itakapopambana na Misri.

Michael Ngadeu-Ngadjui aliutikisa wavu wa Ghana katika dakika ya 72 kwa kufunga bao la kwanza na dakika tatu kabla ya kipenga cha mwisho Christian Bassogog aliyamaliza mashaka yote kwa kuifungia bao la pili timu yake ya Cameroon. Ghana na Burkina Faso zitapambana Jumamosi kuwania nafasi ya tatu. Fainali itachezwa Jumapili katika mji wa Libreville, Gabon.