ACCRA : Rais Köhler ziarani Ghana | Habari za Ulimwengu | DW | 12.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ACCRA : Rais Köhler ziarani Ghana

Rais Hörst Kohler wa Ujerumani amewasili katika mji mkuu wa Ghana Accra kuanza ziara ya siku nne ambapo anatazamiwa kukutana na Rais wa Ghana pamoja na viongozi wengine wa Afrika.

Köhler pia atahudhuria mkutano juu ya mpango ambao ameuzinduwa wa Ushirikiano na Afrika ambao unalenga juu ya njia za kuboresha ushirikiano kati ya Afrika na mataifa yenye maendeleo makubwa ya viwanda duniani.

Ujerumani mwaka huu ni Rais wa Kundi la Mataifa Manane yenye Maendeleo Makubwa ya Viwanda Duniani na imekuwa ikitaka suala la maendelo ya Afrika kupewa kipau mbele na mataifa hayo ya kitajiri duniani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com