Abuja. Mtoto achiliwa huru. | Habari za Ulimwengu | DW | 09.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Abuja. Mtoto achiliwa huru.

Watu wenye silaha nchini Nigeria wamemwacha huru mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitatu raia wa Uingereza ambaye walimteka nyara katika mji wa kusini wa Port Harcourt siku ya Alhamis.

Msemaji wa jimbo la Rivers amesema kuwa Margaret Hill amejiunga na wazazi wake na yuko katika hali nzuri.

Wateka nyara hao walitishia kumuua mtoto huyo iwapo hawatalipwa fedha ama baba yake ambaye ni Muingereza achukue nafasi yake. Polisi wamesema kuwa hakuna fedha zilizolipwa kwa kuachiwa mtoto huyo.

Utekaji kwa ajili ya kujipatia fedha ni jambo linalotokea kila mara katika jimbo linalotoa mafuta kwa wingi la Niger Delta, ambako mji wa Port Harcourt unapatikana , lakini wateka nyara wa mtoto huyo waliwakasirisha hata makundi ya wapiganaji ambao walisema hatua hiyo inadhoofisha juhudi zao za kupata udhibiti mkubwa wa fedha za mafuta yanayochimbwa katika eneo hilo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com