ABU DHABI:Sudan,Chad zafikia muafaka
4 Mei 2007Matangazo
Sudan na Chad zimekubaliana kushirikiana na jeshi la Umoja wa Afrika na lile la Umoja wa Mataifa kurejesha amani, katika eneo la Darfur na la Chad.
Makubaliano hayo yalitiwa saini na na Marais Omar al Bashir wa Sudan na Idriss Deby wa Chad, nchini Saudi Arabia, ambapo walikubaliana kutounga mkono waasi wa nchi hizo.
Pia walikubaliana kuanzisha jeshi la pamoja la mpakani, na kupelekwa kwa waangalizi katika eneo la vita.
Chad inapaka na Sudan katika eneo lenye mzozo la Darfur.Mwezi uliyopita majeshi ya nchi hizo yalipambana katika eneo hilo.