Zuma asema Mbeki si adui wake bali rafiki | Habari za Ulimwengu | DW | 21.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Zuma asema Mbeki si adui wake bali rafiki

JOHANNESBURG:

Kiongozi mpya wa chama kinachotawala nchini Afrika kusini- cha African National Congress-ANC-Jacob Zuma- ameahidi kushirikiana na Rais Thabo Mbeki,mpinzani wake, aliemshinda katika kinyang’anyiro cha kuwania uongozi wa chama hicho jumanne.Zuma ,akifafanua ajenda yake,amesema kuwa ANC itajikita katika sera za siku za nyuma za kutatua tatizo la umaskini.Aidha amesema kuwa ataunga mkono mipango iliozusha mabishano ya ugawaji wa ardhi.Vilevile amegusia hatua ya uwezekano wa kufunguliwa upya mashtaka ya rushwa dhidi yake kufuatia taarifa za mkuu wa ofisi ya mwendesha mashtaka kusema kuwa uwezekano upo.

Mmoja wa washauri wa karibu wa Bw Zuma-Shabir Sheikh, anatumikia kifungo cha miaka 15 jela kwa kuhusika kwake katika kashfa ya rushwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com