1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bukele athibitishwa mshindi katika uchaguzi wa El Salvador

20 Februari 2024

Tume ya uchaguzi nchini El Salvador imetangaza kuwa chama tawala cha Rais Nayib Bukele cha "Nuevas Idea" yaani mawazo mapya kimejishindia viti 54 kati ya 60 vya Bunge kufuatia uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu.

https://p.dw.com/p/4ccAn
Wafusasi wa rais El Salvador
Wafusasi wa Nayib Bukele wa El Salvador wafurahia ushindi wakePicha: Marvin Recinos/AFP/Getty Images

Hii ni baada ya zoezi jipya la kuhesabu kura kufanyika kwa mara nyingine.

Tume hiyo imesema kwamba takriban asilimia 30 ya masanduku ya kura yaliyotumiwa katika uchaguzi wa Urais na Bunge uliofanyika Februari 4, yalihesabiwa upya. 

Rais wa El-Salvador ajitangaza mshindi wa uchaguzi

Rais Bukele amejipatia ushindi wa urais kwa asilimia 84 ya kura huku kukiwa kuliripotiwa hitilafu kadhaa katika mchakato wa kupakia data kwenye mfumo wa kielektroniki.