1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Zardari aapishwa kuwa rais wa Pakistan kwa awamu ya pili

10 Machi 2024

Aliyekuwa mume wa Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Benazir Bhutto, Asif Ali Zardari hii leo ameapishwa kuwa rais wa 14 wa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4dMTE
Rais mpya wa Pakistan Asif Ali Zardari
Mwenyekiti Mwenza wa Chama cha Peoples Party (PPP), Asif Ali Zardari akihutubia wakati wa mkutano wa hadhara kuhusu kifo cha Benazir Bhutto wakati wa maadhimisho ya Miaka 16Picha: PPI/Zuma/picture alliance

Jaji Mkuu Qazi Faez Isa ameongoza kiapo hicho katika hafla iliyofanyika katika makazi ya rais huko Islamabad na iliyoahudhuriwa na viongozi wa kiraia na jeshi.

Zardari, mwenyekiti mwenza wa chama cha Pakistan Peoples, PPP ni kiongozi wa kwanza wa kiraia kuchaguliwa kuwa rais kwa awamu ya pili ya miaka mitano.

Amekiongoza chama hicho cha PPP baada ya mkewe kuuawa katika shambulizi la bomu na risasi mwaka 2007, na kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa rais mwaka 2008.

Hata hivyo awamu yake mpya inaanza katikati ya maandamano kufuatia madai ya wizi katika uchaguzi wa kitaifa wa mwezi Februari, ambapo hakukua na chama kilichopata wingi wa kutosha wa kura.