1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zambia yakabiliwa na mgao mbaya wa umeme kwa masaa 19

Amina Mjahid
19 Desemba 2019

Masaa 19 ya kukatika kwa umeme nchini Zambia kumelemaza shughuli za biashara na maisha ya kila siku. Muda huo bila umeme ndio mrefu zaidi kuwahi kurekodiwa nchini humo.

https://p.dw.com/p/3V6CB
Zambia - Chinesische Entwicklungsprojekte
Picha: DW/A. Jalloh

Ukame katika maeneo ya Kusini mwa Afrika umepunguza kina cha maji kwenye bwawa la umeme la Kariba, ambalo ndio chanzo kikuu cha nishati hiyo nchini Zambia.

Waziri wa nishati wa zambia Mathew Nkhuwa alilieleza bunge wiki iliyopita kwamba kiwango cha maji kwenye bwawa hilo, kimeendelea kupungua na kushuka hadi mita1.48 juu ya kiwango cha chini kabisa cha bwawa hilo kufanya kazi.

Wakaazi wa Zambia wanalazimika kuishi bila umeme kwa takribani masaa 19 au zaidi kila siku, hali ambayo imechochea hasira ya umma.

Mnamo mwezi Novemba kampuni ya taifa ya umeme ZESCO ilianza kuagiza umeme kutoka kampuni ya ESKOM ya Afrika Kusini ili kukabiliana na athari za mgao wa umeme.