MigogoroEthiopia
Zaidi ya watu 50,000 wayakimbia makaazi yao Ethiopia
23 Aprili 2024Matangazo
Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa jana jioni imesema idadi hiyo ya watu ni katika miji ya Alamata, Raya Alamata, Zata na Ofla, tangu Aprili 13.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa hali ya kibinadamu inazidi kuzorota, huku maelfu ya wanawake na watoto wakihitaji msaada mkubwa wa kiutu. Vikosi vya Amhara viliudhibiti mji wa Raya Alamata kusini mwa mji wa Tigray, wakati wa vita vilivyodumu kwa miaka miwili baina ya serikali ya Ethiopia na vikosi vya Tigray.
Chini ya makubaliano ya amani kati ya serikali na mamlaka ya Tigray, vikosi vya Amhara ambavyo viliunga mkono wanajeshi wa shirikisho, vilipaswa kujiondoa kutoka mji wa Raya Alamata baada ya makubaliano hayo kusainiwa huko Pretoria mwaka 2022.