Zaidi ya asilimia 90 Guinea wapiga kura ya 'ndiyo'
23 Septemba 2025
Matangazo
Akizungumza na waandishi habari, Mkuu wa Tume ya Uchaguzi Djenabou Toure amesema kulingana na matokeo ya awali yaliyotangazwa Jumatatu usiku, asilimia 90.06 wamepiga kura ya 'ndiyo' na asilimia 9.04 wamepiga kura ya 'hapana'.
Toure amesema kura hiyo ya maoni ilihitaji takribani asilimia 50 ya wapiga kura ili iweze kupitishwa.
Guinea ni miongoni mwa mataifa yanayozidi kuongezeka Afrika Magharibi ikiwemo Mali, Niger na Burkina Faso ambako jeshi limechukua udhibiti.
Baadhi ya wachambuzi wanasema kura hiyo ya maoni ni njia kwa Jenerali Doumbouya kusaka urais na kuhalalisha utawala wake wa kijeshi.