1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

William Ruto atangazwa kuwa rais mteule wa Kenya

15 Agosti 2022

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC imemtangaza makamu wa rais William Ruto kuwa rais mteule,

https://p.dw.com/p/4FYlv
Kenia Wahlen 2022, William Ruto
Picha: Baz Ratner/REUTERS

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC imemtangaza makamu wa rais William Ruto kuwa rais mteule, kufuatia uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali, akimshinda mwanasiasa wa muda mrefu na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Hata hivyo zoezi hilo limekumbwa na sintofahamu baada ya makamishna wanne wa tume ya IEBC kutangaza kutotambua matokeo ya uchaguzi wa rais wakidai kuwa mchakato huo umekosa uwazi katika hatua za mwisho.

Ruto amepata asilimia 50.49% dhidi ya asilimia 48.8 ya Odinga.