1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaUswisi

WHO: Mkataba wa majanga wakosa kuafikiwa

11 Mei 2024

Nchi 194 wanachama wa Shirika la Afya Duniani WHO zimeshindwa kuafikiana juu ya mkataba uliotafutwa kwa muda mrefu wa kujiandaa kwa majanga

https://p.dw.com/p/4fjv7
Mkuu wa shirika la afya duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus akiwa katika mkutano na waandishi habari mjini Geneva nchini Uswisi mnamo Aprili 7, 2023
Mkuu wa shirika la afya duniani Tedros Adhanom GhebreyesusPicha: Lian Yi/Xinhua/picture alliance

Lengo lililokusudiwa la kile kinachoitwa 'mkataba wa majanga' ni kuidhinishwa wakati wa Kongamano la Afya Duniani mwaka huu, ambalo ndilo chombo kikuu cha maamuzi cha WHO. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Mei.

WHO yatafuta mwafaka juu ya rasimu ya makubaliano

Duru ya hivi karibuni zaidi ya mazungumzo ilianza karibu wiki mbili zilizopita huko Geneva nchini Uswisi na yalielezwa kuwa msukumo wa mwisho wa WHO wa kupata mwafaka juu ya rasimu ya makubaliano iliyoko.

Mazungumzo yalianza miaka miwili iliyopita

Lakini baada ya miaka miwili ya mazungumzo, wanachama hao waWHO, walishindwa kuafikiana kuhusu rasimu hiyo kufikia muda wa mwisho wa jana Ijumaa.

Mojawapo ya maswala yenye utata imekuwa ni iwapo na jinsi gani makampuni ya dawa yanapaswa kulazimika kuelezea utaalamu na kuwezesha sehemu ya bidhaa zao kupatikana kwa nchi maskini.