1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo yamsafisha waziri wa zamani wa afya

Daniel Gakuba
8 Juni 2023

Mahakama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imemuachilia huru Waziri wa zamani wa afya Eteni Longondo, aliyekabiliwa na madai ya ubadhirifu.

https://p.dw.com/p/4SLY4
Pichani ni muuguzi akiandaa dozi ya chanjo ya virusi vya corona ya AstraZeneca katika kituo cha afya cha Ngaliema, mjini Kishansa.
Kongo ilikumbwa na madai ya ubadhirifu wa fedha za kupambana na janga la UVIKO 19. Picha: Hereward Holland/REUTERS

Longondo alikamatwa mwaka 2021 kwa madai ya ubadhirifu wa fedha zilizotengwa kwa ajili ya mapambano dhidi yaUVIKO-19

Longondo, ambaye aliongoza wizara ya afya kuanzia mwaka 2019 hadi 2021, alikuwa akishukiwa na Mkaguzi Mkuu wa Fedha (IGF) kwa ubadhirifu wa zaidi ya dola milioni 7 zilizotengwa kupambana na janga hilo.

Wakili wa Waziri huyo wa zamani, Hugues Pulusi Eka ameliambia shirika la habari la AFP kuwa mteja wake aliachiwa jana na Mahakama ya rufaa ambayo ilihitimisha kwamba hakukuwa na ushahidi wa kumuweka hatiani Bwana Longondo. 

Rais Felix Tshisekedi, aliyeingia madarakani Januari mwaka 2019, ameapa kupambana dhidi ya ufisadi katika uongozi wake.