Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani ataka jeshi kujiandaa na vita
6 Juni 2024Matangazo
Pistorius amesema jeshi la Ujerumani, Bundeswehr linatakiwa kuwa tayari kwa vita ifikapo mwaka 2029. Amesema hayo alipokuwa akijibu maswali ya wabunge jana Jumatano na kuongeza kuwa jeshi hilo linahitaji fedha zaidi, vifaa na wanajeshi watakaokuwa tayari kwa vita.
Amesema, katika hali ya dharura, wanahitaji wanaume na wanawake wenye nguvu watakoweza kulitetea taifa lao.
Pistorius aidha, amesema anadhani kuna sababu ya kuwa na mfumo mpya wa jeshi kama sehemu ya uimarishwaji huo, pamoja na kuiagiza wizara yake kutafuta watu wanaoweza kujiunga na jeshi.
Ujerumani ilisitisha mfumo wa kujiunga jeshini kwa hiyari mwaka 2011, lakini karibu nusu ya Wajerumani wanataka urejeshwe.