1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand Shinawatra aachiwa huru

18 Februari 2024

Waziri mkuu wa zamani wa Thailand Thaksin Shinawatra leo hii ameachiwa huru kutoka gerezani kwa msamaha.

https://p.dw.com/p/4cXfe
Thailands ehemaliger Premierminister Thaksin Shinawatra
Picha: Wason Wanichakorn/AP Photo/picture alliance

Shinawatra mwenye umri wa miaka 74, alikuwa akitumikia kifungo kwa makosa ya rushwa. Vyombo vya habari vya Thailand vilichapisha picha za mwanasiasa huyo aliyerejea kutoka uhamishoni miezi sita iliyopita, akichukuliwa kwenye gari kutoka katika hospitali ya polisi na kurejea nyumbani kwake kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya muongo mmoja.Gazeti la Bangkok Post liliripoti, likimnukuu Waziri wa Sheria, Tawee Sodsong akisema ametimiza vigezo vya kuachiwa kwa msamaha kwa kuwa ana zaidi ya miaka 70, na ana maradhi makubwa lakini pia ametumikia angalau miezi sita yake kifungo chamwakammoja jela.Waziri Mkuu huyo wa zamani alirudi nchini mwake Agosti mwaka jana baada ya kuishi miaka 15 uhamishoni.  Alipowasili tu, alipelekwa Mahakama Kuu na kisha kwenda gerezani, na baadae hospitali ya polisi.