1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaThailand

Waziri mkuu wa zamani wa Thailand ahamishiwa hospitali

23 Agosti 2023

Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand Thaksin Shinawatra amehamishiwa hospitali ya polisi kutoka gerezani mapema Jumatano, ikiwa ni chini ya siku moja baada ya kurejea nchini kutokea uhamishoni.

https://p.dw.com/p/4VTdI
Thailand -Thaksin Shinawatra na familia yake
Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand Thaksin Shinawatra aliporejea kutoka uhamishoniPicha: Athit Perawongmetha/REUTERS

Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand Thaksin Shinawatra amehamishiwa hospitali ya polisi kutoka gerezani mapema siku ya Jumatano, ikiwa ni chini ya siku moja baada ya kurejea nchini kutokea uhamishoni na kuanza kutumikia kifungo chake cha miaka nane.

Thaksin mwenye umri wa miaka 74, aliwekwa jela ili kutumikia vifungo kutokana na hukumu za makosa kadhaa ya uhalifu zilizotolewa wakati akiwa uhamishoni, makosa ambayo alisema yalichochewa kisiasa.

Maafisa wa gereza wamesema Thaksin alisumbuliwa na shinikizo la juu la damu na asingeweza kulala usiku kutokana na maumivu katika kifua chake.

Saa chache baada ya Thaksin kurejea Thailand, mgombea wa chama Pheu Thai Srettha Thavsin alipata kura za kutosha kuwa waziri mkuu mpya, na kuhitimisha kipindi cha karibu miezi mitatu ya mivutano ya kisheria na malumbano yaliyofuatia uchaguzi wa Mei.

Srettha anatarajiwa kuidhinishwa rasmi baadae leo na mfalme wa Thailand kama waziri mkuu mpya.