1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Aliyekuwa waziri mkuu waThailand ahukumiwa kifungo jela

22 Agosti 2023

Mahakama kuu ya nchini Thailand imemhukumu waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Thaksin Shinawatra adhabu ya kifungo cha miaka minane jela.

https://p.dw.com/p/4VRAa
Waziri mkuu huyo wa zamani wa Thailand, Thaksin Shinawatra tayari amewasili jela Jumanne kuanza kutumikia kifungo.
Waziri mkuu huyo wa zamani wa Thailand, Thaksin Shinawatra tayari amewasili jela Jumanne kuanza kutumikia kifungo.Picha: Athit Perawongmetha/REUTERS

Shinawatra alikamtwa saa chache aliporejea nchini humo baada ya kuwa nje kwa muda wa miaka 15.

Mahakama hiyo imesema adhabu aliyopewa inahusiana na hukumu zilizotolewa dhidi yake wakati alipokuwa nje ya nchi.

Makosa yanayomkabili ni pamoja na matumizi mabaya ya mamlaka, kuiagiza benki inayoendeshwa na serikali kutoa mkopo kwa mteja wa nje kinyume cha sheria.

Na pia kosa la kumiliki hisa kinyume cha sheria kwa kuwatumia mawakala binafsi.