1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Waziri Mkuu wa Senegal atangaza serikali yake mpya

Lilian Mtono
6 Aprili 2024

Waziri Mkuu wa Senegal Ousmane Sonko ametangaza serikali mpya itakayokuwa na mawaziri 24 na manaibu 5 siku chache baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.

https://p.dw.com/p/4eUg9
Ousmane Sonko, Waziri Mkuu wa  Senegal
Waziri Mkuu wa Senegal Ousmane SonkoPicha: Sylvain Cherkaoui/AP/dpa

Sonko amesema rais Bassirou Diomaye Faye aliyeapishwa siku ya Jumanne kuiongoza Senegal baada ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa rais wa Machi 24, amewaidhinisha mawaziri wote waliopendekezwa.

Utendaji wa  Baraza hilo jipya la mawaziri utafuatiliwa kwa karibu hasa kutokana na ahadi kubwa za mageuzi zilizotolewa na rais Faye wakati wa kampeni. Miongoni mwa hizo ni kuzifanyia ukaguzi mkubwa sekta za nishati ya mafuta, gesi pamoja na uchimbaji madini.

Miongoni mwa walioteuliwa kuwa mawaziri ni Cheikh Diba atakayeongoza wizara ya fedha na Abdourahmane Sarr atakuwa waziri wa uchumi. Majenerali wawili wameteuliwa kuongoza wizara ya mambo ya ndani na ya Ulinzi.