Waziri Mkuu wa India atembelea maonesho ya Hannover | Matukio ya Kisiasa | DW | 13.04.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Waziri Mkuu wa India atembelea maonesho ya Hannover

Waziri mkuu wa India Narendra Modi ambaye yuko ziarani nchini Ujerumani leo akiambatana na mwenyeji wake Kansela Angela Merkel wameyatembelea maonyesho ya viwanda mjini Hannover

Deutschland Narendra Modi und Angela Merkel auf der Hannover Messe

Waziri Mkuu Narendra Modi na Angela Merkel kwenye maonesho ya Hannover

Mwaka huu India ni nchi mshirika katika maonyesho hayo makubwa kabisa ya viwanda duniani. Zaidi na Mohammed Abdul-Rahman.

Akiyafungua maonyesho hayo ya viwanda ya Hannover,waziri mkuu Modi ameyataka makampuni ya Ujerumani yawekeze nchini mwake.India ni nchi ambako uchumi unakuwa haraka kuliko nchi yoyote ile duniani." Pia akatangaza mageuzi ya kina nchini mwake kuhusiana na masuala ya ushuru,urasimu,fedha na mazingira.India ni mwandalizi mwenza wa maonyesho ya mwaka huu,yanayotajikana kuwa maonyesho makubwa kabisa ya viwanda ulimwenguni. Modi alisema Ujerumani ni mshirika muhimu wa kibiashara kwa India miongoni mwa nchi za Umoja wa Ulaya.

Kuna mataifa 70 duniani

Hannover Messe Eröffnung Merkel Modi

Narendra Modi na Angela Merkel kwenye maonesho ya Hannover

Kiasi ya makampuni 6,500 kutoka mataifa 70 duniani yaanashiriki katika maonyesho hayo katika mji huo wa kaskazini mwa Ujerumani na kuna waawakilishi 400 wa viwanda kutoka India.

Taifa hilo ambalo ni nguvu moja wapo kubwa ya kiuchumi barani Asia linapanga kuitumia nafasi hiyo kuonyesha sura kwamba India ni mahala bora pa uwekezajina pa biashara .

Waziri mkuu wa India anatarajiwa mjini Berlin kesho, ambako atalakiwa kwa heshima kamili ya gwaride la kijeshi kabla ya mazungumzo na Kansela Merkel. Halikadhalika atakutana na Waziri wa uchumi Sigmar gabriel na waziri wa mambo ya nchi za nje Frank-walter Steinmeier . Waziri mkuu huyo anajaribu kuuza kile kinachoitwa " Imetengenezwa India," kampeni aliyoianzisha Septemba 2014 kuyavutia makampzuni ya kigeni kutengeneza bidhaa zao nchini India. Kampeni hiyo inataja juu ya sekta 25 mbali mbali, ikiwa ni pamoja na sekta ya madawa, magari, teknolojia ya habari na utalii. zikitajwa kuwa na nafasi kubwa katika ukuaji uchumi.

Ujerumani ni mshirika mkubwa wa India barani ulaya na biashara ya nchi hizi mbili ilikadiriwa kuwa euro bilioni 16.08 mwaka 2013.

Ziara ya Waziri mkuu wa India barani ulaya ilianzia Ufaransa wiki iliopita ambako alikutana na Rais Francois Hollande na viongozi hao wakatangaza kutiwa saini mikataba kati ya nchi zao mbili ikiwa ni pamoja na India kun unua ndege za kivita za Ufaransa chapa ya Rafale, pamoja na mikataba mkiwili tafauti kuhusiana na mradi wa nishati ya nyuklia huko Jaitapur, kusini magharibi mwa India. Baada ya ziara yake nchini Ujerumani Waziri mkuu wa India narendra Modi ataelekea Canada.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman, dpa

Mhariri:Yusuf Saumu

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com