1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Gerd Mueller kufanya ziara barani Afrika

Sekione Kitojo
21 Agosti 2018

Katika ziara ya mataifa saba katika bara la Afrika ianyoanza Jumatano waziri wa ushirikiano wa maendeleo wa Ujerumani Gerd Mueller atahimiza juu ya eneo la biashara huru na Afrika pamoja na kufurahia mafanikio yake. 

https://p.dw.com/p/33Vss
Bundesentwicklungsminister Gerd Müller
Picha: picture-alliance/dpa/R. Jensen

Biashara  huria  ama  biashara bila  kutoza  ushuru  kwa  muda  mrefu sio  tena  mada  muhimu, kwasababu  kwa  muda  mrefu  bidhaa  kutoka Afrika zimeingia  katika   mataifa  mengi  ya bara  la  Ulaya, amesema mtaalamu  wa  maendeleo  ya  kiuchumi  Robert Kappel  katika mahojiano  na  DW.  Mara  nyingi  mada kuhusu  ruzuku  katika  mazao pamoja  na  vizuwizi  vya  biashara  yamekuwa  masuala yanayozungumzwa sana. Profesa  kutoka  chuo  kikuu  cha  Leipzig anaishutumu  Ulaya  kwa  ukoloni  mamboleo  katika  sera  za  fedha. Mada hii  lakini anaiweka  kando waziri Mueller ,   hususan  wakati huu wa  ziara  yake  katika bara  la  Afrika. Anashindwa kuelewa  kwamba yeye  ndie amepanua  mwanya  wa  kutokuwa  na  usawa  katika biashara  na  kuwa  mkubwa  zaidi  katika  miaka  iliyopita, licha  ya kuwapo uhuru  wa  kutokuwa  na  ushuru.

Gerd Müller in Kenia
Waziri Mueller akiwa katika kambi ya wakimbizi nchini KenyaPicha: picture-alliance/M. Gottschalk/BMZ-Poolfoto

Kappels  amedokeza  kwamba  waziri  hana  taarifa  sahihi na anapaswa  kukosolewa. Uhusiano  wa  kibiashara  baina  ya  Ulaya  na Afrika  unazidi  kukua kinyume  na  manufaa  ya  Afrika. Wakati  katika baadhi  ya  nchi  za  Afrika  bidhaa  zinazoingizwa  kutoka  Ulaya  na hususan  Ujerumani  zinaongezeka  kidogo, mauzo  ya  bidhaa  kutoka Afrika  kwenda  Ulaya  katika  baadhi  ya  nchi  za  Afrka  idadi inapungua.

Hii  inatokana  hususan  katika  suala  la  bei, anasema  Robert Kappel. Kutoka  Afrika bidhaa  inayoingia  katika  mataifa  ya  Ulaya  inakuwa  ni mafuta na  gesi  ya  ardhini kuja  Ujerumani na  mataifa  ya  Ulaya zikifuatiwa  na  mazao ya shambani. Bei ya  mazao  ya  shambani  na pia  mafuta  na  gesi  katika  miaka  ya  hivi  karibuni  zimepungua.  Na ndio  sababu  uwiano  wa  kibiashara  kati  ya  nchi  za  Afrika  na  Ulaya umeingia  katika  hali ya  kutowiana."

Udanganyifu  wa  kibiashara

Kwa mujibu  wa  tarakimu za  shirika  la  mahitaji  ya  kibiashara  la Ujerumani  la  Germany Trade and Invest kulikuwa  na  udanganyifu  wa biashara  ya  nje  ya  Ujerumani  pamoja  na  mataifa  ya  Afrika  kusini mwa  jangwa  la  Sahara  unaofikia  euro  bilioni  26 katika  miaka iliyopita. Kwa  sababu  Afrika  kusini mwa  jangwa  la  Sahara  katika mwaka  2017  kwa   biashara  ya  asilimia  1.1  tu  ilipoteza  sehemu ndogo  ya  biashara  jumla kama  ilivyokuwa  katika  mwaka  mmoja uliopita.

Prof. Dr. Robert Kappel
Dr. Robert Kappel wa taasisi ya mitaala ya dunia mjini LeibnizPicha: Werner Bartsch/GIGA

Kwa dhamira  ya  Umoja  wa  Ulaya  na  pia  serikali  ya Ujerumani, hapo  baadaye  bidhaa  nyingi  zaidi  za  Ulaya  zitaingia  katika  soko  la Afrika. Kwasababu  katika  wakati  huo  mataifa  ya  ulaya  yamegundua kwamba  Afrika  ni  soko  muhimu. Hadi  ifikapo  mwaka  2050 robo  ya wakaazi  wa  dunia  watakuwa  wanaishi  katika bara  la  Afrika , inaeleza taasisi  ya  takwimu  ya  Ulaya, Eurostat.  Afrika  itakuwa  dude kubwa  lililolala katika  uchumi  wa  dunia", wanasema  mjini  Berlin  na Brussels. Na  soko  hili  muhimu  hawataki  kuliacha  bila  mapambano kwa  mikononi mwa Wachina  na  Wahindi. Biashara  na  mataifa  ya Asia  na  Afrika  inaongezeka  kwa  miaka  kadhaa  sasa  na  ina umuhimu  mkubwa  katika  ukubwa  wake.

Tangu  muda  mrefu Umoja  wa  Ulaya  umekuwa  ukifanya  majadiliano na  nchi  za  Afrika  kuhusiana  na  mkataba  mpya wa  kibiashara, unaofahamika  kama  makubaliano ya  ushirikiano  wa  kiuchumi EPA. mkataba  huo  unataka  kufunguliwa  kwa  ukamilifu  masoko kwa  ajili ya  bidhaa  za  Ulaya  katika  soko  la  Afrika. Waungaji  mkono wanamatumaini  kupata  soko muhimu  kwa  pande  zote  mbili, na kuongeza ufanisi  kupitia  ushindani, na bei  za  chini kwa  watumiaji.

Äthiopien Frühstück Abiy und Isaias
Miradi ya maendeleo kutoka Ethiopia ambako waziri Mueller atafanya ziara piaPicha: Fitsum Arega/Prime Minister Office Ethiopia

Katika  ziara  yake ya wiki  moja  waziri Mueller kuanzia  siku  ya Alhamis  atafanya ziara  katika  nchi  saba za  Afrika. Baada  ya Eritrea, Ethiopia, Msumbiji, Botswana, Zimbabwe  na Chad , atamalizia ziara  yake  nchini Ghana.  Katika  mazungumzo  yake  na  kansela  wa Ujerumani  na  rais  wa  Ghana Nana Akufo-Addo  kutakuwa  na  suala la mabadiliko  ya  ushirikiano  kwa  nchi  hizo  mbili  pamoja  na uwezekano  wa  uwekezaji.

Mwandishi: Cascais, Antonio / ZR /  Sekione  Kitojo

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman