1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiJamhuri ya Czech

Watu wanne wafa kwenye ajali ya treni, Jamhuri ya Czech

6 Juni 2024

Watu wanne wamekufa na wengine kujeruhiwa baada ya treni ya abiria kugongana na treni ya mizigo katika mji wa Pardubice nchini Jamhuri ya Czech.

https://p.dw.com/p/4ghvW
ajali ya treni | Pardubice
Behewa la treni lililoacha njia baada ya treni ya abiria kugongana na treni ya mizigo huko Pardubice, Jamhuri ya Czech, Juni 5, 2024 katika picha hii iliyopatikana kutoka kwa mitandao ya kijamii.Picha: Jiri Sejkora/via REUTERS

Msemaji wa idara ya dharura Alena Kisiala amethibitisha idadi hiyo kwa kituo cha televisheni cha Czech.

Ajali hiyo imetokea jana usiku na treni hiyo ilikuwa imebeba abiria zaidi ya 300 wengi wao wakiwa ni wageni. Ilikuwa ikitokea Prague kueloekea mji wa Chop ulioko magharibi mwa Ukraine na unaopakana na Slovakia.

Msemaji wa kikosi cha zimamoto kwenye eneo hilo Vendula Horakova amekiambia kituo hicho kwamba treni ya mizogo ilikuwa inasafirisha Calcium.