1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroBurkina Faso

Makumi wauawa msikitini wakati wa sala Burkina Faso

27 Februari 2024

Watu kadhaa wameuawa kwa kupigwa risasi ndani ya msikiti katika kijiji cha Natiaboni mashariki mwa Burkina Faso.

https://p.dw.com/p/4cv45
Mwanajeshi akishika doria katika kijiji cha Tarikent
Mwanajeshi akishika doria katika kijiji cha TarikentPicha: Sebastien Rieussec/Hans Lucas/IMAGO

Kwa mujibu wa chanzo cha usalama, watu waliokuwa na silaha waliwashambulia waumini ndani ya msikiti majira ya saa kumi na moja alfajiri.

Hata hivyo, ripoti ambazo bado hazijathibitishwa zinaeleza kuwa idadi ya watu waliokufa huenda ikawa kubwa zaidi tofauti na hesabu iliyotolewa na maafisa.

Natiaboni ni kijiji kilichoko takriban kilomita 60 kusini mwa Fada N'Gouma, mji mkuu katika eneo la mashariki mwa Burkina Faso ambao umeshuhudia mashambulizi ya mara kwa mara ya watu wenye silaha tangu mwaka 2018.

Shambulio hilo limetokea baada ya watu wasiopungua 15 kuuawa kufuatia shambulio dhidi ya kanisa katoliki wakati wa misa ya Jumapili katika kijiji cha Essakane kaskazini mwa nchi hiyo.

Maeneo ya ibada na viongozi wa kidini nchini Burkina Faso wamekuwa wakishambuliwa katika hujuma ambazo zinadaiwa kufanywa na makundi ya waasi.