1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu kadhaa wauawa Chad

John Juma
28 Februari 2024

Serikali ya Chad imesema watu kadhaa wameuawa kufuatia shambulizi dhidi ya ofisi ya idara ya usalama wa ndani katika mji mkuu, N’Djamena, ikiwatuhumu wale iliowataja kuwa "wanachama wa upinzani" kuhusika.

https://p.dw.com/p/4czeb
Rais Mahamat Idriss Deby wa Chad.
Rais Mahamat Idriss Deby wa Chad.Picha: Gonzalo Fuentes/REUTERS

Barabara zote kuelekea ofisi ya idara hiyo zimefungwa.

Waandishi wa habari wa AFP wameshuhudia jeshi likipelekwa karibu na ofisi kuu ya chama cha upinzani cha PSF.

Kupitia taarifa yake, serikali ilisema shambulizi hilo lilijiri baada ya mwanachama wa PSF kukamatwa na kushtakiwa kwa kile kilichotajwa kuwa "jaribio la mauaji dhidi ya rais wa mahakama ya juu".

Soma zaidi: Waasi Chad wadai kusogea mji mkuu wa N'Djamena

Shambulizi hilo dhidi ya ofisi za usalama limefanyika siku moja tu baada ya tangazo kwamba Chad itafanya uchaguzi wa rais mnamo Mei 6, ambao Yaya Dillo, kiongozi wa chama cha PSF, na binamu yake Rais Deby Into wanakusudia kugombea.