1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 15 wapoteza maisha kwa maporomoko ya udongo Kongo

Amina Mjahid
15 Aprili 2024

Maporomoko ya udongo kusini magharibi mwa Kongo, yaliyotokana na mvua kubwa yamesababisha vifo vya watu 15 huku wengine zaidi ya 60 wakiwa hawajulikani waliko.

https://p.dw.com/p/4em0Q
Kongo| Athari za mvua
Maeneo mengi ya milima nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo hukumbwa na maporomoko ya udongo msimu wa mvua kubwa.Picha: GLODY MURHABAZI/AFP

Gavana wa mpito Félicien Kiway amewaambia waandishi habari kwamba timu ya waokoaji imetumwa katika jimbo hilo kujaribukuwaokoa manusura zaidi.

Kando na taarifa hizo, Dhedhe Mupasa mbunge wa jimbo la Idiofa amesema siku ya Jumamosi watu 7 walipatikana wakiwa hai karibu na bandari ilioko katika jimbo hilo na kwa sasa wanapata matibabu hospitalini.

Afisa mmoja ametahadharisha kwamba itakuwa vigumu kujua idadi kamili ya watu waliopotea, kutokana na eneo hilo kutumiwa kama soko la wazi siku ya Jumamosi, huku akilielezea eneo hilo la tukio kama mahali pa ubadilishanaji wa biashara ambapo wavuvi wanalitumia sana kuuza samaki na kununua sabuni.