JangaAsia
Watu 126 wafa kwenye mafuriko na maporomoko Nepal
29 Septemba 2024Matangazo
Mvua hizo zilizoanza Alhamisi jioni, zimesababisha uharibifu mkubwa nchini humo, hasa katika mikoa ya mashariki na kati.
Kulingana na msemaji wa polisi wa Nepal, Dan Bahadur Karki, watu 73 wamejeruhiwa vibaya katika mikoa mbalimbali tangu Ijumaa.
Soma pia:Zaidi ya watu 59 wafariki nchini Nepal kufuatia mafuriko
Zaidi ya nusu ya vifo vilitokea katika mji mkuu wa Kathmandu na wilaya zinazouzunguka mji huo, zilizoathirika pakubwa na mafuriko na maporoko ya udongo.
Vyombo vya habari nchini humo vimezielezea mvua mjini Kathmandu kuwa ndiyo mbaya zaidi katika kipindi cha miongo kadhaa.