Watu 11 wauwawa katika mapigano makali Mogadishu. | Matukio ya Kisiasa | DW | 08.06.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Watu 11 wauwawa katika mapigano makali Mogadishu.

Watu 11 wameuwawa leo hii katika mapambano makali kati ya wanajeshi wa Ethiopia wakishirikiana na wale wa serikali ya Somalia dhidi ya waasi wa siasa kali za Kiislam mjini Mogadishu.

default

Mwanajeshi wa serikali ya mpito nchini Somalia.

Kwa mujibu wa mashahidi vikosi vya serikali vikiiungwa mkono na vile vya Ethiopia vilifanya msako katika mtaa wa Wardhigley kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu na kuzusha mapigano ambapo mahasimu walishambiliana kwa kutumia silaha nzito

Waethiopia walifyetua mizinga katika soko la Bakara ambapo inaelezwa kwamba raia wengi waliuwawa.Wanajeshi watatu wa Somalia na mwanamgambo mmoja wameuwawa katika kitongoji cha karibu cha Hararyale ambapo mpigano yaliwa makali sana.

Vikosi vya Ethiopia na vya Somalia pia vimekuwa vikitumia silaha za kutungulia ndege katika mapigano hayo.

 • Tarehe 08.06.2008
 • Mwandishi Mohamed Dahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EFfu
 • Tarehe 08.06.2008
 • Mwandishi Mohamed Dahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EFfu
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com