1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 11 wafa maji Kongo

6 Agosti 2019

Watu 11 wamefariki dunia na wengine kadhaa hawajulikani walipo baada ya boti kuzama katika Mto Lukenye nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

https://p.dw.com/p/3NPYe
Uganda Schiffsunglück Lake Albert
Picha: Getty Images/AFP/M. Siiloni

Watu wengine 16 walisalimika kwenye ajali hiyo ya boti iliyokuwa imejaa watu baada ya kufanikiwa kuogelea na kufika eneo salama kulingana na mwandishi wa habari wa eneo hilo aliyezungumza na shirika la habari la AFP.

Ajali hiyo, ambayo ni mfululizo wa ajali za majini za hivi karibuni nchini Congo, ilitokea katika eneo la ndani lililo na misitu katika mkoa wa Kasai, ambako mito inategemewa kama njia ya usafiri kutokana na ukosefu wa barabara.

Gavana wa jimbo la Kasai, Dieudonne Pieme, alilieleza shirika la habari la AFP kuwa watu wapatao 50 hawajulikani walipo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa eneo hilo, watu wengi waliokuwemo kwenye boti hiyo walikuwa wakielekea mjini Kinshasa.

Ajali za boti zimekuwa zinatokea mara kwa mara kutokana na boti zinazowabeba kujazwa watu na mizigo kupita kiasi.