Watu 10 wauawa DRC kufuatia shambulizi la ADF | Matukio ya Afrika | DW | 08.01.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Watu 10 wauawa DRC kufuatia shambulizi la ADF

Raia wanane wameuawa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia shambulizi linalodaiwa kufanywa na kundi la ADF.

Kiasi  ya  raia  wanane  ikiwa  ni  pamoja  na  jamaa za wanajeshi wameuwawa  katika  mashambulizi  yaliyofanywa usiku  na  watu  wenye  silaha  katika  eneo  tete  la mashariki  mwa  Congo, jeshi  limesema leo.

Watu  wanane  wameuwawa  ikiwa  ni  pamoja  na  wanne ambao  ni  ndugu  wa  wanajeshi, katika  wilaya  ya  Mavivi kaskazini  mwa  eneo  la  Beni, msemaji  wa  jeshi  wa jimbo  hilo  Mark Hazukay  ameliambia  shirika  la  habari  la Ufaransa  AFP.

Polisi  imeweka  idadi  ya  waliouwawa  kuwa  ni  10, baada ya  hapo  kabla  kutangaza  kuwa  waliouwawa  ni  wanane.