1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto wanne waliotoweka kwenye msitu wa Amazon wapatikana.

Zainab Aziz
10 Juni 2023

Watoto wanne wa umri wa miaka 13, 9, 8 na mwaka mmoja waliokuwa wametoweka kwa zaidi ya mwezi mmoja katika msitu wa Amazon nchini Colombia wamepatikana wakiwa hai.

https://p.dw.com/p/4SPzr
Kolumbien | Rettung vermisster Kinder nach Flugzeugabsturz
Picha: John Vizcaino/AP/picture alliance

Watoto hao wamesafirishwa kwa ndege hadi mji mkuu wa Colombia, Bogota mapema hii leo.

Watoto hao walionusurika ajali ya ndege ndogo iliyoanguka katika msitu huo, walisafirishwa kwa ndege ya kijeshi hadi uwanja wa ndege wa kijeshi mjini Bogota mapema leo.

Watoto hao walitolewa mara moja kutoka ndege hiyo kwa machela huku ambulansi zikiwasubiri kuwapeleka hospitali.

Rais wa Colombia Gustavo Petro, jana aliwaambia wanahabari kwamba ni siku ya muujiza baada ya kutangaza kuokolewa kwa watoto hao.

Aliongeza kuwa kwasasa watoto hao hawana nguvu na kwamba wanafanyiwa uchunguzi na madaktari.

Rais huyo pia alichapisha picha katika mtandao wa twitter ulionesha watu kadhaa wengine wakiwa wamevalia magwanda ya kijeshi wakiwa wamechoka, huku wakiwashughulikia watoto hao waliokuwa wameketi katika maturubai jangwani.