WASHINGTON:Ujerumani yaisamehe deni Liberia | Habari za Ulimwengu | DW | 15.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Ujerumani yaisamehe deni Liberia

Ujerumani imetangaza kwamba itaisamehe Liberia deni lote la dola milioni 230.

Tangazo hilo limekuja siku moja baada serikali ya Marekani kusema itafuta deni lake la dola milioni 391 kwa nchi hiyo ilioathirika na vita.Katika taarifa ya mwisho ya mkutano huo wa siku mbili pia imesema kwamba serikali ya Marekani italiomba bunge dola milioni 35 kuisaidia Liberia kulipa malimbikizo yake ya madeni kwa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia.

Liberia inadaiwa malimbikizo ya madeni ya dola bilioni moja na nusu na Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia pekee.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com