WASHINGTON : Rais Bush atakiwa kuwa mwangalifu | Habari za Ulimwengu | DW | 12.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Rais Bush atakiwa kuwa mwangalifu

Wabunge waandamizi wa chama cha Demokratic nchini Marekani wamemtaka Rais George W Bush awe muangalifu juu ya kuishutumu Iran kwa kuchochea umwagaji damu nchini Iraq.

Wabunge hao walikuwa wakizungumza baada ya maafisa wa serikali ya Marekani kusema kwamba wana ushahidi kuwa Iran ilikuwa ikiwapatia silaha wanamgambo wa Kishia wanaowashambulia wanajeshi wa Marekani.Maafisa wa ulinzi wa Marekani wamewaambia waandishi wa habari mjini Baghdad kwamba mabomu hayo yamekuwa yakitumiwa kuwaripuwa wanajeshi wa Marekani ambapo zaidi ya wanajeshi 170 wameuwawa tokea mwezi wa Juni mwaka 2004.Madai ya Marekani kwamba mabomu hayo yanaingizwa kwa magendo kutoka Iran hayakuwezwa kuyakinishwa na duru zilizo huru.

Seneta wa chama cha Demokrat Chris Dodd amesema utawala wa Bush ulijaribu kughushi ushahidi hapo kabla.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com