WASHINGTON: Rais Bush ampongeza rais Musharaf | Habari za Ulimwengu | DW | 11.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Rais Bush ampongeza rais Musharaf

Rais George W Bush wa Marekani amempongeza rais wa Pakistan Pervez Musharaf akisema amepitisha uamuzi wa maana kwa kuahidi kumaliza hali ya hatari, kujiuzulu jeshini na kufanya uchaguzi.

Rais Bush amesema anaamini rais Musharaf atajiuzulu wadhifa wake kama kamanda wa jeshi na atahakikisha uchaguzi unafanyika nchini Pakistan.

´Humchukulia mtu kwa maneno yake mpaka anapokiuka anayoyasema. Nafikiri hilo ndilo unalolihitaji mtu kufanya, yaani mtu anaposema atafanya kitu fulani, la busara ni kumpa nafasi kutimiza ahadi yake.´

Rais Bush amesema jenerali Musharaf aliamua mara tu baada ya mashambulio ya Septemba 11 mwaka wa 2001 nchini Marekani kufanywa, kwamba ataiunga mkono Marekani katika vita dhidi ya magaidi walio nchini Pakistan kwa kuwa anafahamu hatari ya kundi la al Qaeda.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com