WASHINGTON : Pigo maradufu kwa Bush | Habari za Ulimwengu | DW | 24.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Pigo maradufu kwa Bush

Katika kile kinachoonekana kama pigo maradufu kwa Rais George W. Bush wa Marekani repoti ya ujasusi imeelezea mashaka yake makubwa juu ya uwezo wa Waziri Mkuu Nuri al Maliki kuiunganisha nchi yake wakati seneta mashuhuri wa chama cha Bush cha Republican akimuhimiza kuanza kondowa wanajeshi wake kutoka Iraq.

Seneta wa Virginia John Warner amesema Maliki amewaangusha wanajeshi wao kwa kushindwa kuchukuwa hatua za kuleta usuluhishi wa kisiasa ambao ungelisaidia kuleta utulivu nchini Iraq. Amesema Bush anapaswa kutangaza hapo mwezi ujao uondowaji wa kwanza wa vikosi vya Marekani kama njia ya kuichochea serikali ya Iraq kuanza kuchukuwa hatua.

Viongozi wa kisiasa nchini Marekani wamekuwa wakiushambulia vikali uwezo wa Maliki kuiongoza Iraq.

Repoti ya ujasusi ya Marekani pia inakuja baada ya watu 32 kuuwawa katika mapambano kati ya wapiganaji wa Al Qaeda na wanamgambo hasimu wa madhehebu ya Sunni kwenye vijiji karibu na Baquba katika jimbo la Diyala.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com