Washington. Gates kumfahamisha Bush mikakati mipya. | Habari za Ulimwengu | DW | 23.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Washington. Gates kumfahamisha Bush mikakati mipya.

Waziri mpya wa ulinzi nchini Marekani Robert Gates anatarajiwa leo kumfahamisha rais wa Marekani George W. Bush kuhusu mwelekeo mpya kwa ajili ya vita vya Iraq.

Gates amerejea kutoka katika ziara katika eneo la vita , ziara yenye lengo la kutafuta mkakati mbadala wa kupambana na ghasia na kuyaruhusu hatimaye majeshi ya Marekani kuondoka nchini humo.

Gates amekataa kutoa maelezo ya mkakati ambao anaumalizia pamoja na makamanda wa kijeshi lakini amewashutumu viongozi wa kisiasa wa Iraq na jukumu lao la kuchukua uongozi wa usalama wao.

Jeshi la Marekani limeripoti vifo vya wanajeshi watano nchini Iraq wakati wa ziara ya waziri huyo wa ulinzi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com