1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makundi ya wapiganaji yadaiwa kuwauwa wengi mwaka huu DRC

6 Agosti 2020

Zaidi ya watu 1,300 waliuawa katika nusu ya kwanza ya mwaka wa 2020 na makundi ya wapiganaji katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikiwa ni mara tatu zaidi ya kipindi sawa na hicho katika mwaka wa 2019.

https://p.dw.com/p/3gWA7
Kongo Milizen und Helfer CNDP Symbolbild
Picha: Getty Images/U. Sinai

Ripoti iliyochapishwa na Ofisi ya Pamoja ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa - UNJHRO inaonyesha kuwa kati ya Januari na Juni 2020, wapiganaji wa makundi yote yenye silaha walihusika na mauaji ya kiholela ya karibu watu 1,315, wakiwemo wanawake 267 na watoto 165.

Hiyo ilikuwa mara tatu zaidi ya 416 ya vifo vya aina hiyo vilivyoorodheshwa katika nusu ya kwanza ya 2019.

Ongezeko hilo ni kutokana na kuzorota kwa hali ya haki za binaadamu katika mikoa ambayo migogoro inatokota, hasa Ituri, Kivu Kusini, Tanganyika na Kivu Kaskazini.

Mashariki ya Congo imekuwa katika machafuko kwa karibu miongo mitatu, ambapo wakaazi wanahangaishwa na makundi ya wapiganaji.