Wapi zipelekwe takataka za kinuklea? | Magazetini | DW | 10.04.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Wapi zipelekwe takataka za kinuklea?

Mjadala kuhusu wapi zipelekwe takataka za miale ya kinuklea na hatima ya kisa kilichopelekea rais wa zamani wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani kujiuzulu ni miongoni mwa mada zilizogonga vichwa vya habari hii leo

Shehena ya takataka za nuklea ikisafirishwa katika chombo maalum hadi Gorleben

Shehena ya takataka za nuklea ikisafirishwa katika chombo maalum hadi Gorleben

Tuanzie na mjadala kuhusu wapi zihamishiwe takataka zenye miale ya kinuklea ambazo hadi wakati huu zilikuwa zikirundikwa ndani ya mahandaki maalum huko Gorleben."Gazeti la Nordbayerischer Kurier" linaandika:"Waziri wa mazingira Altmeier anataka kulitoa suala hilo tete katika kampeni za uchaguzi mkuu.Kwanza wanaanzisha utaratibu mrefu.Lakini kuna siku itawadia tu ambapo ukweli utadhihiri.Takataka zenye miale ya kinuklea zinahitaji mahala maalum.Si shida kutambua.Kadhia hiyo isiyopendeza inabidi kuakhirishwa kwa muda mrefu kwa namna ambayo jukumu la kuishughulikia litawaponyoka wale wanaoishughulikia hivi sasa.

Gazeti la "Cellesche Zeitung" linakosoa ile hali kwamba tume iliyoundwa kulishughulikia suala la takataka za miale ya kinuklea haina nguvu ya kupitisha uamuzi.Gazeti linaendelea kuandika."Ni vizuri kwamba tume hiyo mpya haijaundwa na wanasiasa peke yao-wawakilishi wa mashirika ya jamii" nao pia wamo.Lisilo zuri lakini ni ile hali kwamba tume hiyo kazi yake ni kutoa ushauri tu.Maamuzi ya mwisho yanapitishwa kama kawaida na bunge la shirikisho-Bundestag na baraza la wawakilishi wa majimbo-Bundesrat.Vuta nikuvute kuhusu wapi zipelekwe takataka zenye miale ya kinuklea,itaendelea kwa hivyo hadi mwaka 2031.

Christian Wulff atafunguliwa kesi au la?

Mada nyengine iliyomulikwa na wahariri wa magazeti hii leo inahusiana na uamuzi wa rais wa zamani wa shirikisho,Christian Wulff wa kukataa kulipa faini ya Euro 20.000 ili badala yake mwendesha mashtaka asimuandame kisheria kwa madai ya "Hongo na mapendeleo".Anataka kulitakasa jina lake anasema.Gazeti la "Badische Neueste Nachrichten" linaandika:"Dhana ya kimsingi inapojitokeza,lazma mwendesha mashtaka aifuatilizie tena bila ya kujali hadhi ya mhusika.Kwa hivyo hakuna haja mtu kujipasua kichwa na kujiuliza kama Wulff alibidi kweli kujiuzulu.Haiwezekani kumuona rais anaendelea na wadhifa wake na huku uchunguzi unafanywa dhidi yake.Hata utaratibu wa kiajabu ajabu wa kugharimia nyumba yake na tabia ya rafiki yake mkubwa wa zamani Glaeseker zingemtia dowa.

Gazeti la "Thüringische Landeszeitung linahisi "watu wote ni sawa mbele ya sheria."Gazeti linaendelea kuandika:"Ule usemi,"wadogo wanaandamwa na wakubwa wakubwa wanaachiwa" haukuwa kweli safari hii.Katika kadhia hii watumishi wa mwendesha mashtaka wamefanya kazi yao ipasavyo-kila kitu kimechunguzwa na matokeo yake yamedhihirisha-si kadhia nzito hivyo.Wulff wakati ule hakuwa na kitu.Hilo si kosa japo kama unapokuwa na cheo hutakiwi kufanya hivyo.Kwamba amefanikiwa akiwa bado kijana kukabidhiwa wadhifa wa rais wa shirikisho-hiyo ni sehemu ya historia ya aina pekee.Ndo kusema kansela hakuwa akijua hali yake ya kifedha ikoje au aliifumbia macho hali hiyo,muhimu zaidi ikiwa kumshinda mgombea wa upande wa upinzani?Masuala yapo,lakini hakuna mahakama itakayoweza kuyajibu.Kwa bahati mbaya.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri:Mohammed Khelef

DW inapendekeza