Wapi Olimpik 2016 ? | Michezo | DW | 02.10.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Wapi Olimpik 2016 ?

Je, ni Chicago; Rio de Jeneiro;Madrid au Tokyo ?

Rais Barack Obama na first lady Michelle Obama

Rais Barack Obama na first lady Michelle Obama

Macho ya ulimwengu yanakodolewa leo mjini Copenhagen,Denmark ambako Halmashauri kuu ya Olimpik Ulimwenguni (IOC), inaamua wapi michezo ya Olimpik ya majira ya kiangazi mwaka 2016 ifanyike .

Miji 4 iko katika kinyan'ganyiro hiki-nayo ni Rio de Jeneiro,jiji kuu la Brazil; Chicaco,Marekani,Real Madrid,Spain na Toyo,Japan, mji pekee kati ya hiyo 4, uliokwisha andaa michezo hiyo, lakini 1964.

Marais na wafalme,mawaziri wakuu na wanaspotri maarufu kama Pele, wamewasili Copenhagen kuipigia debe miji yao. Usoni kabisa ni Rais Barack Obama na mkewe Michelle Obama,wanaotaka kuileta michezo ya 2016 mjini kwao-Chicago:

Jiji la Chicago limetupa turufu zake 2 mezani hii leo-siku ya finali-nazo ni Rais Barack Obama na mkewe Michelle.Wote wawili walitoa hotuba za kusisimua kuutetea mji wao wa Chicago. Rais Obama aliruka kwa ndege usiku wa jana na moja kwa moja alihudhuria Kikao cha Halmashauri kuu ya olimpik Ulimwenguni akijiunga na mkewe Michell.Aliwakumbusha wajumbe kwamba Chicago ni mahala ambapo tangu yeye hata mkewe wanakuita "nyumbani".

Rais Obama alisema na ninamnukulu, " Nimekuja hapa leo kama shabiki mkubwa wa michezo ya Olimpik pamoja na ile ya walemavu na ni mwenye imani kubwa na chama kinachowakilisha michezo hiyo na mkaazi anaejivunia wa Chicao ." Rais Obama , rais wa kwanza wa Marekani, alie madarakani kuwahi kuihutubia Halmashauri Kuu ya Olimpik ulimwenguni akasema,

"Nimekuja hapa kuwataka hii leo, muuchague mji wa Chicago kwa sababu ile ile ilionifanya mimi kuupenda mji huu miaka 25 iliopita na kuufanya maskani yangu."

Michelle Obama, alimfuta mumewe kuwahutubia wajumbe akikumbusha akiwa mtoto mdogo mapajani mwa baba yake akiangalia michezo ya olimpik akivutiwa na ustadi wa wanariadha wa (gymnastics) Olga Korbut , Nadia Comaneci na Carl Lewis.

Lakin,i sio Chicago tu inayoania tiketi ya kuandaa olimpik 2016-baada ya michezo ya London, 2012:Rio de Jeneiro, jiji kuu la Brazil linaania sasa kwa mara ya 4 kuandaa olimpik na kuwa mji wa kwanza kabisa katika Amerika Kusini, kupewa heshima hiyo.

Rais Lula na mfalme wa dimba Pele, wanaupigia nao debe mji wao wa Rio na kwavile michezo hii imezunguka mabara yote isipokua Afrika na Amerika Kusini, wabrazil wanadai ,huu ni mwaka wao kucheza samba Rio.Rais wa IOC ,mbelgiji Jacques Rogge,angejivunia nae sana kwamba kabla hakustaafu 2012 mjini London,amefaulu kuipeleka michezo ya olimpik Amerika Kusini.Jiji la Madrid nalo linapigiwa upatu tangu na mfalme wa Spain,Juan Carlos na hata waziri mkuu Zapatero.

Tokyo, mji mkuu wa Japan nao,haukuachwa mkono na waziri wake mkuu mpya: Tokyo hakuna kitisho kwa usalama,lakini kati ya miji hiyo 4 ,Tokyo umeshaanda olimpik 1964 na mwaka jana tu , michezo hii ilifanyika jirani Beijing,nchini China.Kinyanganyiro kwahivyo, kinatazamiwa jioni hii kati ya Chicago na Rio de Jeneiro. Sitapenda kuagua.

Muandishi: Ramadhan Ali/ AFPE

Mhariri: M-Abdulrahman