1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaonya juu ya kitisho cha wanawake wanaouawa Honduras

25 Aprili 2024

Umoja wa Mataifa umeonya juu ya kile ilichoita "dharura" ya mauaji ya wanawake nchini Honduras, wakati karibu wanawake 66 wakiwa wameuawa hadi sasa kwa mwaka huu pekee.

https://p.dw.com/p/4f9mv
Umoja wa Mataifa waonya juu ya ongezeko la mauaji ya wanawake nchini Honduras
Wanaharakati mbalimbali duniani wamekua wakipambana kupigania haki za wanawake na kutaka visa vya aina hiyo kusitishwaPicha: Fabrizio Zani/ANSA/picture alliance

Mratibu mkaazi wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Amerika ya Kusini Alice Shackelford amesema taifa hilo lina viwango vya juu kabisa vya mauaji ya wanawake.

Amesisitiza mbele ya waandishi wa habari ya kwamba hiyo ni dharura na kuelezea wasiwasi wake kwamba ukatili sasa unaonekana kama jambo la kawaida dhidi ya wanawake. 

Soma pia:Unyanyasaji wa kingono waongezeka mjini Goma, DRC

Karibu visa 380 vya mauaji ya wanawake vilirekodiwa nchini humo mwaka uliopita, imesema Idara inayofuatilia ukatili ya Chuo Kikuu cha National Autonomous cha nchini Honduras.