Wanariadha wawili wa Kenya wako taabani
27 Agosti 2015Matangazo
Shirikisho la Kimataifa la Riadha – IAAF limesema kuwa Koki Manunga na Joyce Zakary wamepigwa marufuku kwa muda baada ya kutumia dawa hizo.
Wanariadha hao wa mita 400 walilengwa kabla ya kushiriki katika mbio hizo katika hoteli yao mnamo tarehe 20 na 21 Agosti kulingana na taarifa hiyo ya IAAF
Shirikisho la Riadha Kenya limethibitisha kuwa limefahamishwa kuhusu vipimo hivyo vya IAAF vilivyobaini matumizi ya dawa za kusisimua misuli dhidi ya wanariadha hao wawili. Taarifa ya AK, imesema tayari shirikisho hilo limekutana na IAAF na wanariadha hao wawili na kuanzisha uchunguzi wa hali iliyosababisha matokeo hayo na hatua muafaka itafuata nchini Kenya.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohamed Khelef