1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo mashariki mwa DRC wauwa watu wapatao 15

Saumu Mwasimba
24 Machi 2023

Wanamgambo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamewauwa kiasi watu 15 katika matukio matatu tofauti ya mashambulizi ya hivi karibuni kabisa katika eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4PAUb
Konflikt im Kongo | M23 Soldaten
Picha: Guerchom Ndebo/AFP

Afisa kutoka shirika moja la kiraia kwa jina Charite Banza amefahamisha kwamba wapiganaji wa kundi la waasi la CODECO walishambulia kijiji cha Drodro katika mkoa wa Ituri kwenye mji wa Djungu siku ya Jumatano.

Watu sita waliuwawa kwa kukatwakatwa kwa mapanga, na wengine watatu waliuawa katika kijiji kingine kilichoko umbali wa kiasi kilomita 30.

Soma pia: DRC: Mauaji dhidi ya raia yanaendelea licha ya uwepo wa vikosi vya usalama

Kwa upande mwingine, wanamgambo wa kundi la Allied Democratic Forces-ADF nao walishambulia jana Alhamisi katika mkoa wa Ituri na kuuwa raia sita, kwa mujibu wa mfanyakazi mmoja wa shughuli za kutoa msaada aliyeomba kutotajwa jina.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Flucht aus Bergkarabach
Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW
Nenda ukurasa wa mwanzo