Wahariri wa magazeti wataka kodi ya mali ianzishwe | Magazetini | DW | 26.04.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Wahariri wa magazeti wataka kodi ya mali ianzishwe

Wahariri wa magazeti leo wanakizungumzia kitendawili cha kiuchumi, jee kubana matumizi ili kuutatua mogogoro wa madeni au inapasa kutumia fedha zaidi ili kuleta ustawi.?

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri wa fedha Wolfgang Schäuble

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri wa fedha Wolfgang Schäuble

Mhariri wa gazeti la "Stuttgarter Nachrichten" Mhariri anakumbusha kwamba sera kutumia fedha imetumika kwa muda wa miaka mingi lakini matokeo yake yamekuwa ni kulimbikiza deni kubwa linalongezeka kila siku.

Mhariri wa gazeti la "Der neue Tag" anasema tokea sera za kubana matumizi ianze kutekelezwa, serikali kadhaa zimeondolewa na wanachi katika nchi zinazotumia sarafu ya Euro. Mhariri huyo anasema, ili kuirejesha imani ya wananchi, serikali za Ulaya zinapaswa kutoza kodi ya mali ili kuchangia katika juhudi za kuutatua mgogoro wa madeni.

Mhariri huyo anaeleza kwamba tokea mgogoro wa madeni uanze mnamo mwaka wa 2008, nusu ya serikali zimeshaondolewa na wapiga kura barani Ulaya. Sababu ni kwamba sera ya kubana matumizi inawabana wananchi zaidi, bila ya kuwapo wizani wa kijamii. Kwa hiyo ili kurejesha imani ya wananchi serikali zinapaswa kuanzisha kodi ya mali kwa kipindi cha muda mrefu ili kuyalipa madeni. Kwani ni kwa kodi hiyo kwamba matabaka yote yatashirikishwa katika kuubeba mzigo wa madeni. Utaratibu huo utarejesha imani ya wananchi juu ya serikali zao.


Gazeti la "Lausitzer Rundschau" linatoa mwito kwa Ujerumani wa kufanya mageuzi ya kiuchumi bila ya kuchelewa licha ya takwimu za kuvutia zinazoenekana sasa. Mhariri wa gazeti hilo anasema takwimu juu ya uchumi wa Ujerumani ni za kuvutia sana kulinganisha na zile za nchi nyingine za Ulaya.Na hali ya siku za usoni pia inaonekena kuwa nzuri sana. Lakini historia imeonyesha kuwa hali kama hizo hufuatiwa na mishuko ya uchumi ,ikiwa hatua sahihi hazichukuliwi katika wakati wa kufaa. Lakini inawawia vigumu wanasiasa wa Ujerumani kutangaza mageuzi. Wanapaswa kutambua kwamba katika nchi nyingine vilevile chaguzi zinafanyika.

Mhariri wa gazeti la "Ludwigsburger Kreiszeitung" pia anawataka viongozi wa Ujerumani watambue kwamba mabadiliko makubwa yanatokea duniani na kwamba wanapaswa kuchukua hatua za kufaa haraka, kabla mambo hayajaenda mrama. Mhariri huyo anahoji katika maoni yake. kwamba China sasa inabadilika kutoka kuwa muagizaji wa bidhaa na kuwa muuzaji wa bidhaa za tekinolojia za juu. Ndiyo kusema katika muda mfupi ujao China pia inaweza kuwa muuzaji wa magari,ndege na mashine. Ujerumani inahitaji mpango wa mwekeleo mpya, kama ule wa agenda 2010 ulioleta mageuzi ya kijamii.

Mwandishi:Mtullya abdu/Deustche Zeitungen/

Mhariri:AbbdulRahman