1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 56,800 wamefariki wakisafiri

Sekione Kitojo
1 Novemba 2018

Idadi kubwa ya wahamiaji wamekufa maji, wamefariki katika jangwa ama wameingia katika mikono ya wasafirishaji haramu, wakiziacha  familia zao kutofahamu kile kilichowasibu. 

https://p.dw.com/p/37VWH
Picha ya maktaba
Picha ya maktabaPicha: Getty Images/C. McGrath

Wakati  uhamiaji  unaongezeka  duniani, hata  vifo  pia vimeongezeka, hayo  yamesemwa  na  shirika  la  kimataifa la  uhamiaji , ambapo  mamia  kwa  maelfu  ya  watu wanaofariki  ama  kupotea  tu  wakati  wa  kufanya  safari hizo  idadi  imeongezeka. 

Idadi  kubwa  ya  wahamiaji wamekufa  maji, wamefariki  katika  jangwa  ama wameingia  katika  mikono ya  wasafirishaji  haramu, wakiziacha  familia  zao  kutofahamu  kile  kilichowasibu. 

Wakati  huo  huo, miili  ya  watu  ambao  hawakutambuliwa inaendelea  kuzikwa  kwa  wingi  katika   makaburi  katika jimbo  la  Gauteng  nchini  Afrika  kusini , ama   katika  mji wa  pwani  nchini  Tunisia  wa  Zarzis.

Makaburi  kama  hayo  pia  yanapatikana  nchini  Italia , Ugiriki  na  Libya. 

Shirika  la  habari  la  Associated  Press limetoa idadi ya  zaidi  ya wahamiaji  56,800  waliofariki ama  kupotea  duniani  kote  tangu  mwaka  2014, ambayo ni  karibu  mara  mbili  ya  idadi  iliyopatikana  katika  juhudi rasmi pekee  ya  kuhesabu  waliofariki  ama  kupotea iliyotolewa  na  shirika  la  Umoja  wa Mataifa  la  shirika  la kimataifa  la  uhamiaji.