Wahamiaji 34 wamekufa maji katika bahari Mediterrania | Matukio ya Afrika | DW | 03.10.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Wahamiaji 34 wamekufa maji katika bahari Mediterrania

Shirika la IOM limesema wahamiaji wasiopungua 34 wamekufa katika ajali ya meli magharibi mwa Bahari ya Mediterrania, ambamo watu 26 wamenusurika

Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM, likinukuu duru za jeshi la majini la Morocco na shirika la misaada la Uhispania, limesema wahamiaji wasiopungua 34 wamekufa katika ajali ya meli magharibi mwa Bahari ya Mediterrania, ambamo watu 26 wamenusurika.

Wizara ya mambo ya ndani ya Morocco imesema watu 31 wameokolewa na kwamba maiti 11 ziligunduliwa siku ya Jumatatu.

Wizara hiyo imesema wahamiaji wote waliokuwepo kwenye boti hiyo walitokea Afrika, Kusini mwa jangwa la Sahara, na kuongeza kuwa mpangaji wa safari hiyo alikuwa raia wa Mali.

Msemaji wa shirika la IOM Joel Millman, ameliambia shririka la habari la Reuters kuwa boti hiyo ilikuwa inalea baharini tangu Jumapili ikiwa na watu 60, na kuongeza kuwa watu wasiopungua 34 walizama na inaonekana kulikuwa na manusura 26.

Amesema taarifa hizo zilitolewa na jeshi la majini la Morocco na shirika lisilo la kiserikali la Uhispania la Caminando Fronteras, au mipaka inayotembea.