Wafugaji Dodoma wadai haki zao
20 Aprili 2017Matangazo
Mkoa wa Dodoma kiasili ni wa wakulima na wafugaji kwani ndio shughuli za asili za kutafuta kipato cha kuendesha maiasha ya kila siku kwa familia mbalimbali.
Kutokana na asili hiyo basi baadhi ya wananchi wamekuwa na wakiendelea na utamaduni wa kufuga pamoja na miji kuendelea kukua na kuwa si rafiki kwa shughuli za ufugaji wa asili kwa maana ya kutoa mifugo na kupeleka maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuipatia malisho kwa maana majani yaani machungani.
DW imezungumza na baadhi ya wafugaji hao ambao wanaonekana kuchukizwa na kitendo cha kukamatwa mifugo wakisema ikiwezekana watengewe maeneo ya kufugia. Mbali na kukamatwa mifugo, lakini pia wanalalmikia juu ya kutozwa faini bila kupewa risti, jambo ambalo anasema huenda ni utapeli